Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Brigedi za Sayyid al-Shuhada nchini Iraq, ametangaza kuunga mkono mkakati wa Yemen wa kuchukua hatua dhidi ya usafiri wa meli kupitia Mlango wa Bab al-Mandab, akisisitiza kuwa eneo la kijiografia la nchi za Mashariki ya Kati lina umuhimu mkubwa katika kudhibiti mishipa muhimu ya biashara ya kimataifa.
Al-Wala’i amesema kuwa falsafa ya kuzuia na kujilinda dhidi ya vitisho (deterrence) haiishii tu katika kumiliki silaha za nyuklia, bali pia inajumuisha kutumia uwezo na nafasi ya kimkakati ya kijiografia ambayo nchi zinamiliki.
Akieleza mshikamano wake na wananchi wa Yemen, kiongozi huyo wa upinzani wa Iraq amesema kuwa wananchi wa Yemen wana haki ya kuchukua hatua ya kufunga Mlango wa Bab al-Mandab, ili kuufanya ulimwengu usikie ujumbe wao na kutambua kwamba “wananchi wa Yemen hawatakufa kimya.”
Kauli hiyo inaonesha kuendelea kuongezeka kwa uungaji mkono kutoka kwa makundi ya upinzani katika eneo kwa hatua za Yemen, ambayo yamekuwa yakisisitiza matumizi ya uwezo wa kimkakati wa kijiografia kama njia ya kuleta shinikizo na kujibu vitisho dhidi ya mataifa ya eneo.
Maoni yako